Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia 6000 wa Sudan Kusini hadi sasa wamesafirishwa nyumbani kutoka Khartoum

Raia 6000 wa Sudan Kusini hadi sasa wamesafirishwa nyumbani kutoka Khartoum

Takriban raia 6000 wa Sudan Kusini wamepata msaada wa kurudi nyumbani kutoka mjini Khartoum kupitia mpango unaoendeshwa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Watu hao ni kati ya wengine 12,000 ambao awali walikuwa wamekwama kwenye mji wa Kosti ulio umbali wa kilomita 300 kutoka mjini Khartoum wakisubiri kusafirishwa nyumbani.

IOM inasema kuwa hadi sasa imefanya safari 40 za ndege zinazowafarisha watu hao kutoka Khartoum kwenda Juba. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE )