Maelfu wakimbia Sudan na kuingia Sudan Kusini

25 Mei 2012

Maelfu ya watu kutoka eneo la milima ya Nuba nchini Sudan wanaendelea kuhama na kuingia nchini Sudan Kusini kufuatia hali mbaya ya usalama katika eneo hilo. Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa idadi ya wakimbizi kwenye kambi ya Yida nchini Sudan kusini imepanda hadi watu 35,000 huku idadi hiyo ikitarajiwa kuzidi watu 40,000 mwishoni mwa mwezi.

Melissa Fleming kutoka UNHCR anasema kuwa wengi wa wakimbizi wanaowasili kambini wana utapiamlo baada ya kutembea kwa siku kadha wakielekea kambi ya Yida.

(SAUTI YA MELISSA FLEMMING)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter