Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kipindi cha mpito nchini Somalia Chaelekea Ukingoni

Kipindi cha mpito nchini Somalia Chaelekea Ukingoni

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga amesema kuwa ratiba imewekwa kuhakikisha kuwa ramani ya amani imetekelezwa kabla ya kumalizika kipindi cha mpito nchini humo.

Akihutubia waandishi wa habari kwenye makao ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi nchini Kenya, Mahiga amesema kuwa mkutano uliondaliwa mjini Addis Ababa nchini Ethiopia uliamua kuwa viongozi wa chadi watakusanyika mjini Mogadishu kwa minajili ya kuwaleta wawakilishi wa wasomali kutoka kila sehemu ya nchi ambao watakuwa na jukumu la kupitisha katiba na kuwachagua wabunge wapya . Mahiga amesema kuwa shughuli hizi zote ikiwemo ya kumchagua rais mpya zitafanyika kabla ya tarehe 20 mwezi Agosti mwaka huu wakati wa kukamilika kipindi cha mpito.

(SAUTI YA AUGUSTINE MAHIGA)