Changamoto Zinazowakabili Wanawake Duniani

Changamoto Zinazowakabili Wanawake Duniani

Katika makala ya wanawake wiki hii tutaanzia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako juma hili limekamilika kongamano la kimataifa la watu wa asili lililojumuisha watu kutoka kila pembe ya dunia. Baadhi ya masuala yaliyogusiwa ni changamoto zinazowakabili wanawake wa asili na mwandishi wetu Joshua Mmali alikutana na Bi Anna Naramat aliyekuwa akiwakilisha jamii ya Wamaasai kutoka Narok Kenya amemweleza masaibu yanayowakumba wanawake wa Kimasaai huko Narok.

(MAHOJIANO NA ANNA NARAMAT)

Tukiondoka New York sasa tuelekee Afrika ya Mashariki nchini Tanzania kwenye eneo la Ulyankulu mkoani Tabora, ambako kumekuwa na kambi kubwa ya wakimbizi wa Kutoka Burundi. Mwandishi wetu George Njogopa aliyekuwa ziarani na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi NHCR amepata fursa ya kukutana na baadhi ya kina mama ambao sasa ni raia wa Tanzania baada ya kuvua hadhi ya kimbi waliyokuwa nayo kwa zaidi ya miongo mitatu

(MAKALA NA GEORGE NJOGOPA)