Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Safari ya kwanza ya Gari linalotumia Umeme kukamilika karibuni Afrika

Safari ya kwanza ya Gari linalotumia Umeme kukamilika karibuni Afrika

Kila mwaka May 28 hapa Marekani ni siku ya makmbusho na kwenye Umoja wa Mataifa ni siku ya mapumziko, na ndio maana leo tnawaletea kipindi maalumu badala ya taarifa zetu za habari kama kawaida. Kipindi hili kinaangazia safari ya kwanza ya aina yake ya gari linalotumia umeme kufanyika barani Afrika.

Tarehe 11 Mai Umoja wa Mataifa ulifanya uzinduzi wa safari hiyo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi ambako ilikuwa kituo cha kwanza cha safari ,ambayo itapitia katika nchi sita.

Lengo kubwa la safari hiyo ya gari lisilotumia mafuta, lisilonguruma wala kutoka gesi chafu ni kuhamasisha kuhusu umuhimu wa nishati isiyoathiri mazingira. Hivi sasa gari hilo bado liko safarini na siku chache zijazo itatia nanga mjini Johanesburg nchini Afrika ya Kusini.

Mwandishi wetu Jason Nyakundi alikuwa shuhuda wetu katika uzinduzi huo na anafuatilia safari inavyoendelea. Msikilize katika kipindi hili maalumu.

(PKG NA JASON NYAKUNDI)