Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa UM wasema hakuna madhara yaliyothihirika moja kwa moja baada ya kujaribika kwa mtambo wa nyuklia nchini Japan

Wataalamu wa UM wasema hakuna madhara yaliyothihirika moja kwa moja baada ya kujaribika kwa mtambo wa nyuklia nchini Japan

Ripoti iliyotokana na utafiti wa awali uliofanywa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa katika vinu za kuzalishia mitambo ya nyuklia nchini Japan imeonyesha pamoja na wafanyakazi wengi waliokuwa kwenye kinu cha Fukushima kukaribiana na miale ya mitambo hiyo, lakini hata hivyo hakuna athari za moja kwa moja zilizobainika.

 Wataalamu hao kutoka kitengo maalumu cha mitambo ya atomic na miale yake, wamesema kuwa baada ya kukusanya taarifa toka vyanzo mbalimbali, hakukuweza kubainika moja kwa moja athari zilizowakumba wafanyakazi hao.

March mwaka uliopita 2011 mtambo wa nyuklia wa Fukushima unaotumika kuzalisha nishati ya umeme uliharibiwa vibaya kufuatia tetemeko kubwa lililoikumba pwani ya Japan.Tetemeko hilo ambalo lilikwenda sambamba na mawimbi ya tsunami lilileta uharibifu mkubwa kwa taifa hilo.

Ilipopita miezi miwili baadaye Umoja wa Mataifa kupitia kamati yake ya sayansi na masuala ya miale ya nyuklia ilianzisha uchunguzi kubaini kama kuna athari zozote kwa maisha ya binadamu zilizosababishwa na matukio hayo.