Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna hofu ya kutimiza Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanayohusu Wanawake na Watoto

Kuna hofu ya kutimiza Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanayohusu Wanawake na Watoto

Umoja wa Mataifa unasema malengo mawili ya maendeleo ya milenia kati ya manane yaani MDG’s ambayo yanahusu afya ya wanawake na watoto huenda yasitimizwe kwa wakati. Malengo hayo namba 4 linalohusu kupunguza vifo vya watoto wachanga na namba 5 ambalo ni upatikanaji wa huduma bora za uzazi ndio yanayosuasua kuliko malengo mengine ambayo kwa mujibu wa maafikiano ya Umoja wa Mataifa na nchi wanachama yanapaswa kutimizwa kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2015.

Mikakati mbalimbali imeanzishwa ili kuzisaidia nchi kutimiza malengo haya muhimu ikiwa ni pamoja na “mkakati wa kimataifa wa afya na wanawake na watoto”, mradi wa mwaka 2010 uitwao “Kila mama, kila mtoto” na tume ya habari na uwajibikaji kuhusu afya na wanawake na watoto ya mwaka 2011. Dr Flavia Bustreo ni naibu mkurugenzi wa afya ya familia, wanawake na watoto.

(SAUTI YA DR FLAVIA BUSTREO)