Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali za Asia-Pacific zatoa wito wa kuchagiza Uchumi

Serikali za Asia-Pacific zatoa wito wa kuchagiza Uchumi

Serikali za Asia-Pacific zimetoa wito wa kuchukuliwa hatua ili kuimarisha mahusiano ya kikanda ya kichumi, biashara na nishati kama nguzo muhimu kwa ukauji wa uchumi sik uza usoni hasa ikizingatiwa changamoto zilizopo.

Maazimio kadhaa yamepitishwa wakati nchi hizo zikihitimisha mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa wa tume ya uchumi na jamii kwa nchi za Asia Pacific ESCAP.

Mkutano huo uliokamilika May 23 umetoka na ajenda ya kujumuisha wadau wote katika kanda kwa lengo la kuziba mapengo ya maendeleo miongoni mwao na kupiga hatua za uchumi unaojali mazingira. Katibu Mkuu wa ESCAP Noleen Heyzer ameziambia nchi hizo 49 kwamba kwa pamoja zitaweza kubadili maazio waliyoweka kuwa vitendo na kuzaa matunda wanayoyatarajia.