Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa kuboresha Ushirikiano wa Mataifa ya Kusini Kusini wazinduliwa

Mpango wa kuboresha Ushirikiano wa Mataifa ya Kusini Kusini wazinduliwa

Umoja wa Mataifa umezindua tovuti yenye wajibu wa kuboresha mawasiliano. Tofauti hiyo ambayo italeta ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea ilizinduliwa juma hili na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP mjini New York Marekani.

Naibu mkurugenzi mkuu wa UNEP Amina Mohammed anasema kuwa mawasiliano ya mtandao ni muhimu katika kubadilishana mawazo. Watu na mashirika wanaohusika na masusla ya mazingira kwenye nchi zinazoendelea wamekaribishwa kubadilisha maoni na ujuzi wao kupitia tovuti hiyo.