Serikali ya Afrika Magharibi lazima kukomesha Usafirishaji Haramu wa Watoto:Ezeilo

24 Mei 2012

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu usafirishaji haramu wa watu, hasa wanawake na watoto, Joy Ngozi Ezeilo, ametoa wito kwa serikali ya Gabon ilishughulikie kwa kina swala la kuwasafirisha watoto kutoka Afrika Magharibi na Kati wanaoingizwa nchini humo. Bi Ngozi pia ameihimiza serikali hiyo kuyazingatia maswala ya desturi za kitamaduni ambazo huchangia kuendelezwa kwa tabia hiyo ya usafirishaji na utumwa.

Mtaalam huyo ambaye amekuwa akiizuru Gabon tokea Mei 14 hadi 18, amesema kuwa ikiwa Gabon itatimiza wajibu wake katika kulivalia njuga swala hili, basi itakuwa mfano wa kuigwa na mataifa mengine katika eneo zima. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter