Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma za Upatanishi ni lazima zitolewe Haraka kwa wanaozihitaji:Ban

Huduma za Upatanishi ni lazima zitolewe Haraka kwa wanaozihitaji:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kwamba mataifa yote yanayohitaji huduma za upatanishi za Umoja wa Mataifa ni lazima yaweze kupata huduma hizi pale yanapozihitajim kwa haraka na kwa njia rahisi.  Ban amesema haya wakati wa kikao kisicho rasmi cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu wajibu wa mataifa wanachama katika upatanishi.

Ban ameyapongeza mataifa hayo kwa kulipa kipaumbele swala la upatanishi, na kwamba kikao hicho cha Baraza Kuu ni hatua muhimu katika juhudi za pamoja kwa ajili ya amani, na kwamba pia kinaweza kuchangia vyema mpango wa miaka mitano wa utendaji wa Umoja wa Mataifa. Amemsifu pia mwenyekiti wa Baraza Kuu kwa juhudi zake hasa kwenye kikao alichokisimamia mwezi Januari, ambacho kilichangia sana azimio la mwaka 2010 kuhusu upatanishi.

Katibu Mkuu ameongeza kuwa serikali huchukua nafasi muhimu katika upatanishi wa kimataifa, na kuchangia upatanishi kama majirani wa nchi zilizoathiriwa na mizozo.