Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa Umoja wa Mataifa waonya Mataifa ya Asia Kuhusu Miradi Mikubwa ya Kilimo na Haki za Wenyeji

Wataalam wa Umoja wa Mataifa waonya Mataifa ya Asia Kuhusu Miradi Mikubwa ya Kilimo na Haki za Wenyeji

Wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa kuhusu chakula na watu wa kiasili, wametoa wito kwa mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia yasikandamize haki za jamii za eneo hilo, ambazo hupata moja kwa moja riziki na tamaduni zao kutokana na mazingira yao ya kiasili.

Wataalam hao, wakiwa ni Mtaalam Maalum wa Maswala ya haki ya lishe, Olivier De Schutter, na yule wa maswala ya watu wa kiasili, James Anaya, wamesema kuwa viongozi wa mataifa ya eneo hilo wasishawishike na ahadi za wawekezaji wa miradi mikubwa wakati wanapokagua umiliki wa ardhi kwa ajili ya mazao ya kilimo yanayouzwa ngambo na nishati itokanayo na mimea. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)