Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO yaanzisha ulinzi kwa raia baada ya kuzuka machafuko mashariki wa DRC

MONUSCO yaanzisha ulinzi kwa raia baada ya kuzuka machafuko mashariki wa DRC

Vikosi vya ulinzi wa amani na usalama vya Umoja wa Mataifa vinavyoendesha operesheni yake ya amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC vimechukua jukumu la kuanzisha ulinzi kwa maisha ya raia kufuatia kuzuka kwa mapigano katika jimbo la Kivu Kaskazini upande wa mashariki mwa nchi hiyo ambako kiongozi wa zamani wa waasi anadaiwa kuendesha vitendo vya kiharamia.

Kiongozi wa waasi Bosco Ntaganda ndiye anayetajwa kupalilia machafuko katika eneo hilo akipata uungwaji mkono toka kwa kundi la waasi la FARDC.

Kwa mujibu wa msemaji wa MUNUSCO Roger Meece hali ya wasiwasi inayomwandama kiongozi huyo wa waasi anayetakiwa na mahakama ya kimataifa uhalifu wa kivita ndiyo iliyochochea kuanzisha vurumuai za kivita.

Mwendesha mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC Luis Moreno Ocampo amesema kuwa anasaka hatua mpya kuongeza mashtaka kwa kiongozi huyo yanayohusiana uhalifu dhidi ya binadamu.