Baraza la Usalama, Ban walaani shambulizi la kigaidi Yemen

22 Mei 2012

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likiungwa pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, limelaani shambulizi la kigadi la lililotokea katika mji wa mkuu wa Yemen Sanaa ambalo liliuwa kiasi cha askari 96 na kujeruhi watu 300.

Akilaani vikali shambulizi hilo, Ban amesema kuwa matukio ya mwenendo huo kamwe hayavumiliki tena yanabeba sura ya kinyama na kuchukiza. Ametoa mwito akitaka wahusika wote kwa shambulizi hilo wanaletwa kwenye mkono wa haki.

Taifa hilo la Yemen kwa sasa lipo kwenye mapitio ya mageuzi ya kisiasa kufuatia maandamano makubwa yaliyojitokeza mwaka uliopita yaliyotaka kubalishwa kwa mwenendo wa kisiasa.

Katika hatua yake ya kulaani shambulizi hilo, baraza la usalama pamoja na kuelezea hali ya huruma kwa wale wote waliofikwa na tukio hilo lakini limetaka kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kuwabana wahusika wake.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter