Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bokova afanya mazungumzo na Princess Sumaya kutoka Jordan

Bokova afanya mazungumzo na Princess Sumaya kutoka Jordan

Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO amefanya majadilino na binti wa kifalme Sumaya bint El Hassan kutoka Jordan ambapo walizungumzia mkutano wa Rio + 20 na masusla ya maji , nishati ya jua utafiti na elimu ya sayansi kwenye eneo la nchi za kiarabu.

Sumaya alizungumzia jitihada zinazofanywa na himaya ya kifalme ya Hashemite nchini Jordan kwenye mchango wake katika kuushtawisha uliwmwengu. Pia amezungumzia kujitolea kwake katika kuhakikisha kuwa vijana wenywe vipawa wanawawezeshwa kwenye nyanja za masusla ya sayansi na kwenye uvumbuzi wa kisayansi.