Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahiga asikitika na mapigano yaliyotokea eneo la Somaliland

Mahiga asikitika na mapigano yaliyotokea eneo la Somaliland

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga ameelezea hisia zake kutokana na mapigano yaliyoripotiwa kwenye mji wa Hargeisa eneo la Somaliland mwishoni mwa juma kati ya vikosi vya Somaliland na raia ambapo watu kadha waliuawa.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari ni kwamba mahama moja ya kijeshi kwenye mji wa Hergeisa iliwahukumu vifo raia 17 kutokana na makosa ya kushambulia kituo cha kijeshi kufuatia tofauti kuhusu ardhi. Mahiga amejutia kuuawa kwa watu kutoka pande zote mbili ambapo ametaka kesi hizo kuhamishwa kwenye mahaka zinazohusika na uhalifu ili kuhakikisha kuwa hukumu zinatolewa kwa njia ya haki na pia kutaka uchunguzi wa kina kufanywa kuhusiana  na tukio hilo.