Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa Baraza la Usalama wazuru Afrika ya Magharibi

Ujumbe wa Baraza la Usalama wazuru Afrika ya Magharibi

Ujumbe wa Baraza la Usalama uko ziarani Afrika ya Magahribi kufuatilia na kujadili masuala mbalimbali. Akizungumza katika kituo cha kwanza cha ziara yao nchini Liberia balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice amesema wanatarajiwa kutambua hatua zaidi zitakazochukuliwa na serikali ya taifa hilo ili kuongeza ujuzi na matarajio ya ajira kwa vijana ambao wameathirika na vita na wanaotafura ujuzi na nafasi za kazi kwa ajili ya kujikimu kimaisha.

Pia amesema wamewachagiza Waliberia na serikali kushughulikia changamoto za usalama na kuendelea kujenga uwezo wa masuala ya haki na sekta za usalama. Naye Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf amesema lengo ni kutathimini nchi hiyo ilipofikia hasa katika msaada inaopokea kutoka vikosi vya Umoja wa Mataifa UNMIL, kuona hatua iliyopigwa katika maendeleo, kuelewa changamoto walizonazo ikiwemo mambo ya vijana, miundombinu na maridhiano.

(SAUTI YA SUSAN RICE)