Mkutano wa wawakilishi wa jamii za kiasili kote duniani wamalizika New York

18 Mei 2012

Mkutano wa wawakilishi wa jamii za kiasili kote ulimwenguni, umemalizika leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York. Mkutano huo ambao umekuwa ukifanyika chini ya kamati ya kudumu ya Umoja wa Mataifa kuhusu maswala ya kiasili, umezingatia maswala ya haki za bindamu na mazingira, elimu, utamaduni, maendeleo ya kijamii na uchumi, pamoja na afya na jinsia.

Joshua Mmali amezungumza na Agnes Leina kutoka Kenya, anayeiwakilisha jamii ya Wafugaji, yaani Laramata, ambaye amemwambia kwanza ni nini alichoiga kutoka kwenye mkutano huo…

(SAUTI YA AGNES LEINA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter