Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dhuluma za kimapenzi zatumika kuwatisha watu nchini Colombia:Wahlstrom

Dhuluma za kimapenzi zatumika kuwatisha watu nchini Colombia:Wahlstrom

Mjumbe maaalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhuluma za kimapenzi Margot Wahlström amesema kuwa makundi haramu yaliyojihami nchini Colombia yanatumia dhuluma za kimapenzi kuwatisha watu kwenye sehemu yanakoendesha oparesheni zao.

Hii ni baada ya ziara aliyofanya nchini Colombia na habari alizopokea kutoka kwa wanawake waliobakwa kwenye eneo la Meta lililo umbali wa kilomita 100 kutoka mji mkuu Bogota. Akikamilisha zaiara yake Bi Wallstrom aliyasema haya kutokana na yale aliyoyashuhudia nchini Colombia.

(SAUTI YA MARGOT WAHLSTROM)