Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kufanya uchunguzi kuhusu kutumika kwa mamluki nchini Libya

UM kufanya uchunguzi kuhusu kutumika kwa mamluki nchini Libya

Kundi la Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya mamluki linatarajiwa kufanya ziara nchini Libya kuanzia may 21 hadi 25 kukagua madai ya kutumika kwa mamluki wakati taifa hilo lilipokumbwa na mzozo na hatua ambazo zimechukuliwa na serikali.

Kundi hili la wataalamu huru ndilo litakuwa la kwanza kutumwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa nchini Libya. Kiongozi wa Kundi hilo Faiza Patel anasema kuwa kando na kuchunguza madai ya kutumika kwa mamluki waatalamu hao watajaribu kufahamu shughuli za makampuni ya kibinafsi yanayotoa huduma za ulinzi, shughuli zao nchini Libya na athari kwa haki za binadamu. Joshua Mmali na taarifa kamili.

(SAUTI YA JOSHUA MMALI)