Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Karibu waangalizi 260 watumwa Syria

Karibu waangalizi 260 watumwa Syria

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Syria UNSMIS meja jenerali Robert Mood amesema kuwa ujumbe huo unatarajiwa kufanikisha wajibu wake. Akiongea na waandishi wa habari kwenye mji mkuu Damascus meja Mood amesema kuwa kuna karibu waangalizi 260 wa Umoja wa Mataifa kutoka karibu nchi 60. Meja Mood amesema kuwa ujumbe huo unaendelea kufanikiwa kwenye wajibu wake.

(SAUTI YA GENERAL ROBERT MOOD )

Amesema kuwa wajibu wa kumaliza ghasia nchini Syria unaweza tu kuafikiwa ikiwa kila upande unaohusika kwenye mzozo huo ndani na nje mwa nchi utajitolea kuyapa fursa mazungumzo.