Jaji wa mahakama ya ECCC ajiuzulu wadhifa wake

17 Mei 2012

Mmoja wa majaji kwenye mahamakama inayosikiliza kesi za mauaji ya halaiki nchini Cambodia ECCC na inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa amejiuzulu wadhifa wake. Motoo Noguchi kutoka Japan alimfahamisha katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kuhusu kujiuzulu kwake na kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu.

Chini ya makubaliano yaliyotiwa sahihi kati ya Umoja wa matifa na serikali ya Cambodia mahakama hiyo huru ilibuniwa ikiwahusisha wafanyikazi kutoka Cambodia na wengine kutoka mataifa ya kigeni. Mahakama ya ECCC imetwikwa jukumu la kuwahukumu waliohuska na mauaji ya kimbari na uhalifu mwingine chini ya utawala wa Khmer Rouge miongo mitatu iliyopita.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter