Bragg aelezea wasiwasi uliopo kuhusu hatma ya wapalestina waliohamishwa makwao

17 Mei 2012

Naibu katibu mkuu wa masusla ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Catherine Bragg ameelezea hofu iliyopo kuhusiana na hatma ya wapalestina waliodhiriwa na hatua za Israel za kutwaa ardhi yao wakiwemo waliobomolewa nyumba zao ambapo ametaka kufutiliwa mbali kwa sera zinazowanyima haki ya kujitgemea.

Akiongea baada ya kukamilisha ziara ya siku tatu kwenye maeneo yaliyotwaliwa ya wapalestina Bragg amesema kuwa vitendo kama hivyo ni mateso kwa mwanadamu ni kinyume na sheria za kimataifa na pia ni lazime vikome. Akiwa eneo hilo Bragg alitembea jamii kadha na kushuhdia athari za kutwaliwa kwa ardhi hizo zikiwemo za ukosefu wa usafiri na mahitaji mengine muhimu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud