Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utawala nchini waomba kumfungulia mashtaka Saif Al- Islam

Utawala nchini waomba kumfungulia mashtaka Saif Al- Islam

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC Luis Moreno Ocampo amesema kuwa utawala nchini Libya umeifahamisha mahakama hiyo kuwa unataka kumfungulia mashtaka mwana wa raias wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi kuhusiana na uhalifu uliotendwa wakati kulipoibuka mapunduzi nchini humo.

Kwenye ripoti yake ya mwisho kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kama mwendesha mashataka mkuu wa ICC Ocampo amesema kuwa mahakama hiyo iliwatambua watu watatu kama wahusika wakuu kwa uhalifu uliotekelezwa nchini Libya. Ocampo amesema kuwa watatu hao ni pamoja na rais wa zamani Muammar Gaddafi aliyeuawa na wapiganaji wa upinzani mwezi Oktoba mwaka uliopita, mwanawe Saif Al-Islam na aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini Libya Abdullah Al-Senussi.