Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Burundi wajivunia uraia wa Tanzania

Wakimbizi wa Burundi wajivunia uraia wa Tanzania

Wiki hii serikali ya Tanzania imetangaza kuwapatia uraia wakimbizi zaidi wa Burundi wapatao 54,000 ambao wako katika kambi ya Bulyahulu Mkoani Tabora. Wakimbizi hao waliingia Tanzania katika miaka ya 1970 wakikimbia machafuko yaliyozuka nchini mwao.

Pia serikali ya Tanzania imetoa uraia kwa wakimbizi wengine kadhaa waliko katika kambi za Katumba na Kishamo mkoani Rukwa Kaskazini mwa nchi hiyo. Hii ni mara ya pili wakimbizi wa waliokuwa kwenye makambi ya Tanzania wanapatiwa uraia baada ya kuishi nchini humo miaka mingi.

Mwandishi wetu George Njogopa ameambatana na ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhdumia wakimbizi UNHCR katika kambi ya Ulyahulu mkoani Tabora na amebahatika kuzungumza na watu mbalimbali waliokuwa wakimbizi kutoka Burundi ambao sasa wanajivunia kuitwa raia wa Tanzania. Ungana naye katika makala hii

(FEARURE NA GEORGE NJOGOPA)