Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maambukizi ya HIV kwenye makazi ya wakimbizi wa Burundi yaongezeka

Maambukizi ya HIV kwenye makazi ya wakimbizi wa Burundi yaongezeka

Kazi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika makazi wanayoishi waliokuwa wakimbizi wa zamani wa Burundi huko Ulyankulu Mkoani Tabora imevuka rekodi na kutishia mustabala wa raia hao ambao sasa wamepatiwa uraia rasmi wa Tanzania.

Tayari wataalamu wa afya wameonya kuwa iwapo kutakosekana utashi wa dhati kukabili kwa haraka kasi hiyo basi huenda eneo hilo likashuhudia hali mbaya katika kipindi kifupi kijacho.

Mwandishi wetu George Njogopa kwa wiki nzima sasa yuko kwenye ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhdumia wakimbizi UNHCR katika kambi ya Ulyankulu mkoani Tabora na kutuletea taarifa hii.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)