Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaisaidia Tanzania kukagua viwango vya Carbon katika misitu yake

FAO yaisaidia Tanzania kukagua viwango vya Carbon katika misitu yake

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO, linawasaidia wanasayansi na serikali ya Tanzania kukagua ni kiasi gani cha kaboni kilichoko kwenye misitu na udogo wake, ili kuwasaidia kupunguza gesi za greenhouse zenye kuchafua mazingira. Udongo unaopatikana katika misitu huwa na kiasi kikubwa mno ya kaboni.

Kukata miti, kuharibu misitu au kutodhibiti vizuri matumizi ya misitu kunaweza kuifanya kaboni kuvuka na kuingia angani, na hivyo kuchangia ongezeko la joto duniani. Kwa sababu hizi, ni muhimu kukagua na kuhakiki viwango vya kaboni kwenye udongo na jinsi viwango hivi vinabadilika. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKNDI)