Syria imeshindwa kushiriki katika Tume dhidi ya Mateso

16 Mei 2012

Dunia imeshuhudia idadi kubwa ya vifo na mateso mfululizo nchini Syria, ukiacha mbali idadi ya watoto ambao wameteswa na kuuawa katika hali ya kutisha na kusikitisha huku sluhu ya kisiasa iliyokuwa ikisubiriwa haijapatikana hadi sasa. Kauli hiyo imetolewa Jumatano na Essaida Belmir mtaalamu wa tume hiyo ambaye ni mwakilishi mwenza wa Syria kwenye tume ya kupinga utesaji inayoendelea na kikao mjini Geneva.

Kikao hicho kinatathimini hali ya Syria na hatua zinazochukuliwa na taifa hilo kuhakikisha kwamba inatimiza wajibu wake na ktekeleza mkataba wa kimataifa wa kpinga utesaji, na ukatili mwingine, vitendo vya kinyama au udhalilishaji na adhabu zisizostahili. Amesema muda unatoweka na utu wa watu na aminifu wa mfumo wa Umoja wa Mataifa unategemea sana kupatikana kwa suluhu ya mgogoro wa Syria. Claudio Grossman mweketiki wa kamati amesema kutokuwepo kwa ujumbe wa Syria katika kikao hicho inasikitisha kwani kamati ingefaidika na maoni yao.

(SAUTI YA CLADIO GROSSMAN)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud