Kesi ya Mladic yaanza kusikilizwa ICTY

16 Mei 2012

Kiongozi wa zamani wa Kijeshi wa Kiserbia, Ratko Mladic amefikishwa kwenye mahakama ya kimataifa mjini Hague, Uholanzi kuihusu nchi ya zamani ya Yugoslavia.

Mladic anasifika kama shujaa kwa WaSerbia, na katili kwa WaCroatia. Bwana Mladic anakabiliwa na mashtaka ya mojawepo ya makosa maovu zaidi katika bara la Ulaya tangu vota vikuu vya pili.

Mladic, mwenye umri wa miaka 70, na ambaye ndiye wa mwisho kwa watu muhimu zaidi katika vita vya eneo la Balkan miaka ya tisini. Anakabiliwa na jumla ya makosa kumi na moja, yalotokana na vitendo vyake kama kamanda wa jeshi la Kiserbia katika vita vya Bosnia vya mwaka 1992 hadi 95, yakiwemo mauaji ya kimbari, vitendo vya kigaidi na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Mladic amekataa kujibu mashtaka, ingawa sasa aonekana mdhoofu zaidi kiafya, tofauti na alivyokuwa wakati wa vita.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter