Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha makubalino ya kumaliza mgomo wa kutokula unaofanywa na wafungwa wa kipalestina nchini Israel

UM wakaribisha makubalino ya kumaliza mgomo wa kutokula unaofanywa na wafungwa wa kipalestina nchini Israel

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye mpango wa amani wa mashariki ya kati Robert Serry amekaribisha makubaliano yaliyoafikiwa yenye lengo la kumaliza mgomo wa kutokula unafanywa na wafungwa wa Palestina walio kizuizini nchini Israel. Zaidi ya wafungwa 1000 wa kipalestina walianza mgomo wa kutokula mnamo tarehe 17 mwezi Aprili kupinga kukamatwa kwao , kuzuiliwa kinyume na sheria na hali mbaya ya magereza.

Kwa majuma kadha sasa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na maafisa wengine wa ngazi za juu kwenye Umoja wa Mataifa wamekuwa wakisisitiza umuhimu wa kuzuia kuendelea kuzoroteka kwa hali ya wafungwa wa Kipalestina walio kizuizini nchini Isreal.