Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Al-Nasser atoa heshima kwa waliopinga Utumwa na Biashara ya Utumwa

Al-Nasser atoa heshima kwa waliopinga Utumwa na Biashara ya Utumwa

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nasser ametoa heshima zake kwa wale waliopinga utumwa na biashara ya utumwa akisema kuwa ulimwengu ni lazima ufanye jitihada za kuzuia masuala kama hayo. Akizungumza kwenye tamasha moja la kuunga mkono ujenzi wa makao ya ukumbusho kama heshima kwa waathiriwa wa utumwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Al Nasser aliwapongeza wanawawake na wanaume majasiri waliopinga utumwa na badaye kupata uhuru.

Tamasha hilo linahusiana na siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathiriwa wa utumwa na biashara ya utumwa iliyoadhimishwa tarehe 25 mwezi Machi iliyokuwa na kauli mbiu “kuwakumbuka mashujaa, wapinzani na manusura.”