Ubaguzi na ubaguzi dhidi ya wageni bado unaendelea:Sidibe

15 Mei 2012

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya Ukimwi UNAIDS Michele Sidibe amesema ubaguzi na ubaguzi dhidi ya wageni bado unaendelea katika baadhi ya nchi. Sidibe ameyasema hayo katika ujumbe maalumu wa siku ya kimataifa kupinga ubaguzi na ubaguzi dhidi ya wageni ambayo huadhimishwa May 14. Sidibe amesema mwaka jana dunia imeshuhudia mabadiliko makubwa ya watu kukubali mchanganyiko na wengine, kumekuwa na majadiliano mapya ya uwazi na kuvumiliana.

Hata hivyo amesema bado kuna mataifa na nchi 79 duniani zina sheria ambazo zinaharamisha uhusiano wa watu wa jinsia moja sharia hizi ni kikwazo kikubwa katika vita dhidi ya ukimwi na zinawasukuma kando mashoga, wasagaji, wanaoshiriki mapenzi ya jinsia zote na waliobadili jinsia ambako si rahisi kupata huduma za kuokoa maisha yao.

Amesema thamani ya jamii isipimwe kwa uwezo wa fedha au madraka bali kwa jinsi inavyothamini watu wake bila kujali hisia zao za kimapanzi .Sidibe amewataka watu hao ambao wanabaguliwa katika jamii kujua kwamba UNAIDS iko pamoja nao.Na ametaka watambue kwamba ushiriki wao ni muhimu katika kufikia malengo ya maambukizi mapya ya hiv sufuri,ubaguzi sufuri, na vifo sufuri vitokanavyo na ukimwi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter