Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IPU yakaribisha ripoti za kuhamishwa kwa wafungwa wa kipalestina waliotengwa

IPU yakaribisha ripoti za kuhamishwa kwa wafungwa wa kipalestina waliotengwa

Chama cha kimataifa cha wabunge IPU kimekaribisha ripoti kwamba wafungwa wa kipalestina walio kwenye mgomo wa kutokula na ambao wametengwa kwenye magereza ya Israel watarejeshwa magereza ya kawaida kufuatia makubaliano ambayo huenda yakamaliza mgomo wa kutokula unaoendelea kwenye magereza ya Israel.

IPU pia inataka mfumo wa kuwakamata na kuwafunga bila kuwafungulia mashtaka ambao kwa sasa umewaathiri karibu wapalestina 300 wakiwemo wabunge 24 kutupiliwa mbali kabisa. IPU imerejelea wito wake wa kutaka wanaozuliwa kuachiliwa mara moja au kufikishwa mahakamani kuambata na mipango ya kawaida ya mahakama.