Waalgeria wachagua idadi kubwa ya wanawake bungeni

15 Mei 2012

Jumla ya wanawake 145 wamechaguliwa kama wabunge kwenye uchaguzi uliondaliwa juma lililopita nchini Algeria. Kulingana na chama cha kimataifa cha wabunge IPU ni kwamba Algeria ndilo taifa la kwanza kwenye ulimwengu wa kiarabu iliyo na zaidi ya asilimia 30 ya wanawake bungeni ikilinganishwa na bunge liloondoka ambapo wanawake walichukua asilimia nane tu bungeni. Jemini Pandya ni msemaji wa chama cha IPU na anasema kuwa Algeria kwa sasa inaorodheshwa kuwa moja ya nchi zenye idadi kubwa ya wanawake bungeni kote duniani.

(SAUTI YA JEMINI PANDYA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter