Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Tanzania yatoa Uraia kwa Wakimbizi

Serikali ya Tanzania yatoa Uraia kwa Wakimbizi

Serikali ya Tanzania imetangaza kuwapatia uraia wakimbizi zaidi wa Burundi wapatao 54,000 ambao wako katika kambi ya Bulyahul Mkoani Tabora. Wakimbizi hao waliingia Tanzania katika miaka ya 1970 wakikimbia machafuko yaliyozuka nchini mwao.

Pia serikali ya Tanzania imetoa uraia kwa wakimbizi wengine kadhaa waliko katika kambi za Katumba na Kishamo mkoani Rukwa Kaskazini mwa nchi hiyo. Mwandishi wetu George Njogopa ameambatana na ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhdumia wakimbizi UNHCR katika kambi ya Ulyahulu mkoani Tabora na kutuletea taarifa hii.