Ban apongeza kuondolewa kwa wanajeshi wa Sudan Kusini kutoka Abyei

14 Mei 2012

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha uamuzi wa taifa la Sudan Kusini kwa kuwaondoa wanajeshi wake kutoka kwenye eneo linalozozaniwa la Abyei. Ban amezishauri Sudan na Sudan kusini kukubaliana kuhusu usimamizi wa eneo la Abyei ili kutuliza hali ya eneo hilo. Aidha amezitaka nchi hizo mbili kurejelea mazungumzo nchi ya kamati ya muungano wa nchi za kiafrika AU.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilibuni kikosi cha kulinda usalama katika eno la Abyei cha UNISFA mwezi Juni mwaka uliopita kufuatia mapigano yaliyosabaishwa na hatua ya Sudan ya kulidhibithi eneo hilo na kusabaisha maelefu ya watu kuhama makwao.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter