Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yalaani mauaji ya ya mwanachama wa baraza la amani na uiano

UNAMA yalaani mauaji ya ya mwanachama wa baraza la amani na uiano

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani mauaji ya Arsala Rahmani ambaye ni mwanachama wa baraza la amani nchini humo ukisema kuwa utaendelea kuunga mkono jitihada za kuleta uiano na amani nchini Afghanistan.

Kwenye ujumbe wake UNAMA imetuma rambi rambi kwa familia ya bwana Rahmani ukisema kuwa alijitolea katika kuleta amani na uiano nchini Afghanistan. UNAMA inasema kuwa kisa kama hicho hakikwezi kuvunja moyo walio nao wanachama wa baraza hilo kwenye jitihada za kufanikisha amani na uiano nchini Afghanistan.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari watu waliokuwa na bunduki walimpiga risasi na kumuua Rahmani alipokuwa ndani ya gari lake akielekea kazini magharibi mwa mji mkuu Kabul. Mauji haya yanajiri baada ya yale ya raias wa baraza hilo Burhanuddin Rabbani mwaka uliopita.