Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inatafuta maoni ya wataalamu kwa ajili ya uainishaji wa magonjwa

WHO inatafuta maoni ya wataalamu kwa ajili ya uainishaji wa magonjwa

Kwa mara ya kwanza wataalamu katika sekta ya afya ya jamii ambao wanafanya kazi ya uchunguzi wa wagonjwa na matibabu wana fursa ya kuchangia katika maendeleo ya nyaraka ya kimataifa ya uainishaji wa magonjwa ambao unachapishwa na shirika la afya duniani WHO.

Uainishaji huo ni wa kuhakikisha kwamba Nyanja zote za afya ya jamii na maradhi yanatambulika kwa kila njia. WHO inatoa toleo bora zaidi ambalo litakuwa la 11, na litakaloruhusu maoni ya wadau wote kuongezwa baada ya kufanyiwa tathimini. Na toleo la mwisho linatarajiwa kutoka mwaka 2015. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)