Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yapanga kuwarudisha nyumbani raia wa Sudan kusini

IOM yapanga kuwarudisha nyumbani raia wa Sudan kusini

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa shughuli ya kuwarudisha nyumbani raia wa Sudan Kusini ambao wamekwama kwenye mji ulio kusini mwa mji mkuu wa Sudan Khartoum inatarajiwa kung’oa nanga mwishoni mwa wiki hii.

Raia hao wa Sudan Kusini wamekwama kwenye mji wa Kosti kwa karibu mwaka mmoja wakisubiri kupata usafiri kwenda Sudan kusini. IOM inasema kuwa shughuli hiyo itagharimu dola milioni 5.5. Msemaji wa IOM Jumbe Omar Jumbe anasema kuwa fedha zinahitajika ili kUkodisha mabasi 25, kugharamia safari 100 za ndege na kununuA chakula na madawa na pia kuwatafutia makao wanaorejea nyumbani.

SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE