Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu huru wa UM kutathmini athari za E/IMF Latvia

Mtaalamu huru wa UM kutathmini athari za E/IMF Latvia

Mshauri huru wa haki za binadamu kwa Umoja wa Mataifa, Cephas Lumina, atazuru Latvia kati ya Mei 14 na 18 mwaka huu, ili kukagua athari zinaotokana na mzigo deni la kimataifa la nchi hiyo na mdororo wa uchumi dhidi ya haki za binadamu na haki ya kujiendeleza , pamoja na ufikiaji wa malengo ya Milenia ya Umoja wa Mataifa katika nchi hiyo.

Bwana Lumina atakagua athari za mpango wa Muungano wa Ulaya na Shirika la Fedha Duniani, IMF wa kurekebisha hali ya uchumi wa nchi hiyo dhidi ya kuwepo haki zote za kibinadamu, hasa zile za kiuchumi, kijamii na za kitamaduni.

Bwana Lumina atakutana na maafisa wa serikali, pamoja na mashirika ya kimataifa, zikiwemo taasisi za kifedha. Atakutana pia na wawakilishi wa mashirika ya kutetea haki za binadamu, pamoja na wasomi.