Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wa Mali wanakabiliwa na mapigo mara tatu yaonya UNICEF

Watoto wa Mali wanakabiliwa na mapigo mara tatu yaonya UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limeonya kuhusu kuwepo kwa ukiukaji mkubwa wa haki za watoto nchini Mali, ambako watoto hao hawakumbwi tu na janga la njaa katika eneo zima la Sahel, bali pia tatizo la ukimbizi litokanalo na vita vya waasi.

Naibu Mwakilishi Mkuu wa UNICEF nchini Mali, Frederic Sizaret amesema kuwa watoto wengi sana wanakumbwa na tatizo la utapia mlo, kulazimika kuhama, kutokwenda shule, na sasa kuna habari za kuaminika kuwa haki zao zinakiukwa. Flora Nducha na ripoti kamili

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)