Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mgomo wa kula kwa wafungwa wa kipalestina unatia hofu:UNRWA

Mgomo wa kula kwa wafungwa wa kipalestina unatia hofu:UNRWA

Kamishna Mkuu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Filippo Grandi ameelezea hofu yake kuhusu hali ya afya ya maelfu ya wafungwa wa kisiasa wenye asili ya Palestina wanaofanya mgomo wa kutokula katika magereza ya Israel.

Kamishna huyo ametoa wito kwa serikali ya Israel kutafuta suluhisho mwafaka, akitaja kuwa matakwa ya wale wanaogoma yanahusiana kwa jumla na haki msingi za wafungwa, kama ilivyo kwenye kanuni za Maazimio ya Geneva.

Filippo Grandi amesisitiza wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa wale ambao wamezuiliwa wapelekwe kuhukumiwa au waachiliwe huru, huku akisema, wawili kati ya wafungwa hao wamo katika hali mbaya baada ya zaidi ya siku 74 za mgomo wa kutokula, na huenda wakafariki dunia.