Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visiwa vidogo vinavyochipua kimaendeleo vyakusudia kuachana na mpango wa matumizi ya nishati za kikale

Visiwa vidogo vinavyochipua kimaendeleo vyakusudia kuachana na mpango wa matumizi ya nishati za kikale

Kiasi cha visiwa 20 vinavyoanza kupiga hatua kimaendeleo vimetangaza kuanza kuachana na mpango wa kutegemea dhana za kale kukabili changamoto za kimaendeleo na wakati huo zimeelezea nia ya kukabiliana na tatizo la umaskini.

Wakikamilisha mkutano wa kimataifa ulioangazia suala la matumizi ya nishati mbadala uliandaliwa na Umoja wa Mataifa na serikali ya Barbados, wajumbe kwenye mkutano huo wameongeza kusema kuwa wakati umefika wa kwa mataifa hayo kuanchana na nishati ya kale.

Mataifa hayo yamekamilisha mkutano huo kwa kutoa tamko linalojulikana kama “tamko la Barbados” ambalo linaweka zingatia juu ya ulindaji wa mazingira na kukaribisha maendeleo mapya ya matumizi ya nishati mbadala. Mataifa hayo yameelezea pia hatua za msingi zinazopaswa kuchukuliwa ili kufikisha kwenye ukomo tatizo la umaskini na kufufua njia mpya za ukuzaji uchumi.