Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka majadiliano zaidi kabla ya kufanyika kwa mkutano wa Rio+20

Ban ataka majadiliano zaidi kabla ya kufanyika kwa mkutano wa Rio+20

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewatolea mwito viongozi wa dunia kuongeza majadiliano ili kufanikisha mkutano wa kimataifa unaotazamiwa kufanyika mwezi ujao, mkutano unaojulikana kama Rio +20.

Ban ametaka mataifa pamoja na wahisani wengine kuijadili kwa kina taarifa ya kimaendeleo itayotolewa kwenye mkutano huo unaozingatia agenda ya maendeleo endelevu ili hatimaye shabaha yake itimie kwa wakati.

Amesema zikiwa zimesalia siku 40 kabla ya kufanyika kwa mkutano huo dunia inapaswa kutambua karata ya ushindi bado inashikiliwa hivyo ni vyema siku hizo zilizosalia zikatumika vyema. Ameyasema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu mjini New York na kuongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa ishara ya kutia matumaini lakini hata hivyo bado maamuzi magumu na makini yanapaswa kufanywa sasa.