Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ashauri upunguzaji wa vikosi vya amani Liberia

Ban ashauri upunguzaji wa vikosi vya amani Liberia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amependekeza upunguzwaji wa awamu kwa vikosi vya kulinda amani vilivyoko nchini Liberia katika kipindi cha kuanzia sasa hadi mwaka 2015.

Ameshauri kupunguzwa kwa vikosi 4,200 katika kipindi cha awamu tatu hatua ambayo itafanyika ifikapo mwaka 2015 askari wataosalia nchini humo kufikia 3,750.

Amesema hayo kwa kuzingatia hali ya usalama nchini humo akisema tofauti na ilivyokuwa hapo kabla, kwa sasa Liberia haikabiliwa na changamoto zozote za kiusalama.

Hata hivyo amesisitiza kuwa bado taifa hilo linakabiliwa na changamoto za hapa na pale kuhusiana na hali ya usalama, lakini amesema kitisho cha vikosi vya kijeshi hakiko tena.