Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asilimia 80 ya Wamarekani wasema ni muhimu kuendelea kushikilia nafasi muhimu katika UM

Asilimia 80 ya Wamarekani wasema ni muhimu kuendelea kushikilia nafasi muhimu katika UM

Zaidi ya watu wanane kati ya kumi raia wa Marekani wapiga kura wamesema ni vyema Marekani kuendelea kushikilia nafasi muhimu katika Umoja wa Mataifa, huku asilimia sitini wakisema ni muhimu Marekani kuendelea kutoa mchango wake kwa hazina ya Umoja wa Mataifa mapema.

Waliohojiwa ni watu kutoka vyama vyote na wale wasioegemea chama chochote. Hii inaonesha jinsi ilivyo muhimu kwa Marekani kutojitenga wakati huu.

Kwa maswala ya amani na usalama, kuendeleza afya ya kimataifa na kutoa nafasi sawa kwa wanawake na wasichana- hasa katika kukomesha ndoa za watoto wadogo- Wamarekani wanaamini kuwa Maerekani ni sharti ichukuwe nafasi ya uongozi, na kwamba inaweza kufanya hivyo tu kupitia Umoja wa Mataifa.