Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaitaka Somalia kuwabana wauwaji wa mwandishi wa habari

UNESCO yaitaka Somalia kuwabana wauwaji wa mwandishi wa habari

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ameitaka Somalia kuwashughulikia kisheria wale wote waliohusika na mauwaji ya mwandishi mmoja wa habari aliyekuwa akifanya kazi na kituo cha radio Bwana Farhan James Abdulle.

Mwandishi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 27 aliuawa May 2 mwaka huu na kundi la watu wenye silaha katika kijiji cha Garson kilichoko katikati ya Somalia.

Alikuwa akifanya kazi na kituo cha radio ijulikanayo Galkayo. Kifo cha mwandishi huyo kinafanya idadi jumla ya waandishi wa habari waliouwawa katika kipindi cha mwaka huu pekee kufikia 5.