Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR na wasi wasi wake kuhusu hali ya wafungwa wa kipalestina nchini Israel

OHCHR na wasi wasi wake kuhusu hali ya wafungwa wa kipalestina nchini Israel

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imeelezea wasi wasi wake kutokana na hali ya wakimbizi wa kipalestina walio kwenye mgomo wa kutokula kwenye magereza ya Israel ikisema kuwa inafahamu kuwa baadhi ya wafungwa wako kwenye hali mbaya.

Ravina Shamsadani kutoka ofisi hiyo anasema kuwa kuzuiliwa kwa watu kutoka utawala wa mwingine kunaweza tu kutumiwa nyakati maalumu na kutokana na sababu za kiusalama huku wale waliofungwa wakiwa na haki ya kupinga kufungwa kwao kwa njia ya sheria.

Kamati ya haki za binadamu inasema kuwa kunahitajika kufanyika kwa kesi zilizo huru na zinahitaji kuendeshwa kwa njia ya haki huku haki za kisiasa zikitumiwa kwenye mahakama za kiraia na kijeshi.