Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaanza kusambaza madawa kwa wahamiaji wanaowasili Haradh, Yemen

IOM yaanza kusambaza madawa kwa wahamiaji wanaowasili Haradh, Yemen

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limeanza kusambaza huduma muhimu ikiwemo darzeni za madawa na vifaa vingine vya utibabu kwa mamia ya wananchi walioko huko Haradh nchini Yemen, eneo ambalo linapakana na Saudia Arabia.

Msaada huo wa madawa umetolewa na serikali ya Italia kupitia shirika lake na mashirikiano. Ikishirikiana na serikali ya Yemen, IOM inasambaza misaada ya aina mbalimbali katika maeneo ya Haradh, Abyan, na Al Jawf ambako ndiko kuna idadi kubwa ya watu waliokosa makazi kutokana na mikwamo ya kisiasa.

Kuwasili kwa misaada katika eneo la Haradh kunatizamwa kama hatua muhimu ya kuwahami wakazi wa eneo hilo hasa wakati huu idadi kubwa ya wahamiaji wanaotoka Pembe ya Afrika wakiongezeka. Kuna wasiwasi mkubwa wa kuzuka kwa magonjwa ya mlipuko kutokana na mkusanyiko mkubwa wa watu ambao wanakosa huduma muhimu.