Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuchagiza ajira ni muhimu kwa Rais wa Ufaransa:ILO

Kuchagiza ajira ni muhimu kwa Rais wa Ufaransa:ILO

Wananchi wa Ufaransa wamemkabidhi Rais Francois Hollande mtu wa kwanza kutoka chama cha Kisoshalist kushika madaraka tangu mwaka 1995. Hollande ambaye kampeni zake zililenga serikali kuchagiza zaidi kuliko hatua kali, anashika hatamu za nchi hiyo kukiwa na asilimia 10 ya ukosefu wa ajira.

Afisa wa shirika la kazi duniani ILO Raymond Torres amesema kutoka katika mtego na kuelekea katika ukuaji na mikakati imara ya ajira itakuwa muhim sana kwa Ufaransa hasa wakati ikijaribu kupambana na matatizo ya upngufu wa ajira unaoathiri zaidi vijana. Torres amesema kuwa Rais huyo mpya wa Ufaransa Hollande cha muhimu hivi sasa ni kukuza nafasi za ajira na kuhakikisha kuna mikakati maalumu ya kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Ufaransa ina watu zaidi ya milioni 2.6 wasio na ajira kwa mujibu wa takwimu za karibuni za shirika la ILO, na takribani asilimia 22 ya vijana wenye umri wa miaka 15-25 hawana kazi nchini humo.